Sala kwa Roho Mtakatifu

Njoo, Roho Mtakatifu, Jaza moyo wangu na zawadi zako takatifu.  Nijaze nguvu zako ninapopata udhaifu wowote  siku hii ya leo, nitie nguvu niweze kufanya kazi zinazonikabili na nifanye yaliyo halali na haki.

Nifanye niwe na upendo nisiweze kumkosea au kuumiza hisia za mtu yeyote kimwili ama kiroho, nijalie ukarimu wa kusamehe kwa dhati pale ninapokosewa.

Eh Roho Mtakatifu, Nipe nguvu ninapopata majaribu, nipe nuru katika ujinga wangu,  nipe shauri katika mashaka yangu,  niimarishe katika udhaifu wangu, nisaidie katika mahitaji yangu yote , nilinde katika vishawishi na nifariji katika mateso yangu.

Kwa neema nisikilize Ehe Roho Mtakatifu , na nimwagie mwanga wako ndani ya moyo wangu, roho yangu na mawazo yangu. Nisaidie kuishi maisha matakatifu , na kukua  katika wema na neema

Njoo ndani yangu, Roho Mtakatifu, ili mawazo yangu yote yawe matakatifu. Ingia ndani yangu, Roho Mtakatifu, ili kazi yangu, pia, inaweza kuwa takatifu. Vutia moyo wangu, Roho Mtakatifu, ili nipende tu kile kitakatifu. Nitie nguvu, Roho Mtakatifu, ili nipate kulinda kila kitu kitakatifu. Nilinde, Roho Mtakatifu, ili nipate kuwa mtakatifu daima.

Amina