Sala ya Kujitakasa – Ee Mungu, uniumbie moyo safi

Ee Bwana Mungu,

Asiyetawala roho yake Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako; Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi; 

Ee Bwana, uhimidiwe, Unifundishe amri zako. Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako; Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu; Wala kuifuatisha namna ya dunia hii; bali niugeuze kwa kufanywa upya nia zangu, nipate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu; Dhambi isitawale ndani ya mwili wangu upatikanao na mauti, hata nikazitii tamaa zake; Nisaidie Ee Bwana , nizikimbie tamaa za ujanani; nikafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi; Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako; Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;  Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. Amina

Mithali 25:28, Zaburi 119:10-12, 19:14, 101:3a, 51-10, Warumi 6:12, 2 Timotheo 2:22, Zaburi 119:37. 139:23, 51-7

4 thoughts on “Sala ya Kujitakasa – Ee Mungu, uniumbie moyo safi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.