Tafakari

“… na lolote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake , na kuyatenda yapendezayo machoni pake” (1 Yohane 3:22), “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa” (Yahane 15:7).

Kuomna ni swala Muhimu, Tunaona mistari hiyo miwili inaonyesha umuhimu wa kuomba, Yesu mwenyewe anasisitiza kuomba, kwa maneno mengine, hatupaswi kukaa kimya na kusema Mungu anajua tunayohitaji, ingawa ni kweli Mungu anajua yote lakini ni wajibu kumwita Mungu kwa kuomba.

Lililo kuu ni kushika amri zake na kukaa ndani ya Yesu, hayo ndiyo masharti makuu ili tupate yale tunayoomba.

Karibu katika tafakari hii ili kujua kwa undani misingi na kanuni za kuomba. JE UMEOMBA?

=================================================================================

“Msihukumu, Nanyi hamtahukumiwa…” Luka 6:37

Siku moja nilipokuwa katika shughuli zangu za kila siku, nilipita katika mtaa fulani hapo kinyerzi, nilikutana na kundi la watu, nilipotazama vizuri niakona moshi unafuka katikaki ya kundi la watu hao, na niliona tairi ambayo ilikuwa ikiwaka moto na alikuwa amevikwa mtu akiungua, nilipouliza kuna nini zaidi, nikaambiwa huyo ni kibaka alikuwa amemwibia mtu fulani mahali hapo… polisi walipofika walikuta mtu huyo ameugua vibaya.. hii ndiyo namna watu wanavyojichukulia mamlaka mikoni mwamo na kumhumu huyu mtu bila kujua undaji wake, leo tunaambiwa katika ule mstali wa 37, msihukumu, nanyi hamtahukumia, kuna matukio mengi kama haya na wengi tunapenda kuwahukumu watu kwa yale wanayoyatenda bila kutafakari undaji wa jambo lenyewe, hivyo ni vema katika kila jambo kuliangalia vema na kutokuwahukumu wengine, kwani siku ya mwisho nasi tutahukumiwa.

Lakini vilevile Yesu anatutaka tusiwe tuaangali makosa ya wenzetu tu bila kujipima sisi wenyewe tuanaishi namna gani katika kumpenda Mungu na wenzentu, anatoa mfano wa mtu mwenye  kibanzi na boriti, kibanzi ni kama kijiti kidogo ambacho kinaweza kikakuziba katika jicho lako usione vizuri, na boriki ki kitu kikubwa zaidi ambacho nacho kinaweza kukuziba jicho, sasa kama mtu anafanya kosa fulani,  inabidi ujipime wewe kwanza, je wewe ni safi, maisha yako kiroho ni mazuri,  je unaweza kumsafisha mwenzako?, au una mlaumu na kumsema vibaya wakati wewe nawe una makosa makubwa zaidi. Hivyo katika maisha yetu ya kila siku tusiwe wepesi wa kuangalia makosa ya wengine, bila kuangalia makosa yetu wenyewe. Tusiwe kama wale wafarisayo waliomleta mwanamke aliyekuwa amefumaniwa akizini (katika yohane 8:1-11), na wakamwambia Yesu, sheria inasema apigwe mawe, lakini Yesu aliwaambia yeyote asiye na dhambi na awe wa kwanza kutupa jiwe, na walipojichunguza dhamiri zao wakaona mmmh, hapa sio kwema wote wakaondoaka.

Basi mpendwa ni vema kumwomba Mungu, atujalie tuishi maisha yaliyo ya kujichunguza sisi wenyewe na kuishi kikristo zaidi, bila kuwahukumu na kuwalaumu wengine

4 thoughts on “Tafakari

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.