Mwimbieni Bwana, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.
Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu.
Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake.
Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu.
Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu;
Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, Bwana ametamalaki;